Shirika la kutetea uzuiaji wa Ugonjwa wa kifua kikuu Ulimwenguni (ACTION) ni muungano wa mashirika ya mawakili wa ulimwengu wanaofanya kazi ya kutafuta fedha za matibabu na uzuaji wa uenezaji wa kifua kikuu, ugonjwa ambao unaua mtu mmoja kwa kila sekunde ishirini.
Tangu lianzishwe mwaka wa 2004, vikundi ambavyo vinashirikiana na ACTION vimekuwa vikifanya kazi na mashirika saidizina pia nchi ambazo zimeadhirika sana na ugonjwa wa kifua kikuu ili waongeze fedha zitakazosaidia kumaliza upungufu wa madawa ya ugonjwa huo.
ACTION kwa muda huu inafadhiliwa na Bill & Melinda Gates Foundation.